Vyama vya upinzani vya nchini Uingereza vinajiandaa kuamua kama viunge mkono wito wa Waziri Mkuu Boris Johnson wa kuitishwa uchaguzi mkuu kabla ya wakati au viendelee kumpa shinikizo waziri mkuu huyo.
Kiongozi wa Chama kikuu cha Upinzania cha Labour Jeremy Corbyn anazungumza na viongozi wa vyama vyote ya kisiasa kuhusu kura iliyopangwa kuitishwa wiki inayokuja bungeni, ambapo upande wa upinzani unataka kuwa na uhakika kwamba Waziri Mkuu Boris Johnson hataoondoa Uingereza katika Umoja wa Ulaya bila ya maridhiano ifikapo Octoba 31.