Utekelezaji wa Mikopo asilimia nne kwa Vijana.

Halmashauri ya Jiji la Tanga imetoa mkopo wa pikipiki kwa Vijana sabini kutoka katika kikundi cha Tanga One Youth group kwaajili ya shughuli za kusafirisha abiria maarufu kama bodaboda ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi kupitia utoaji wa mikopo kwa vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.

Akiwakabidhi pikipiki hizo Mkuu wa Mkoa Tanga MARTINE SHIGELA amewataka wanufaika wa mikopo hiyo kuifanyia kazi na kurejesha fedha kwaajili ya kuwapa fursa na wengine.

MUSTAPHA SELEBOSI ni Mwenyekiti wa Kamati ya fedha yeye akaelezea namna watendaji wanavyotekeleza majukumu yao huku Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii DORA NTUMBO akielezea mkopo huo walioutoa kwa kikundi hicho.

Katika hatua nyingine pia kikundi hicho cha vijana kimepatiwa mafunzo maalum kwaajili ya kuzingatia sheria za usalama barabarani.

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwa ni hitimisho la ziara ya Mkuu wa Mkoa Tanga aliyoifanya kwa lengo la kutembelea kata zote ndani ya wilaya ya Tanga.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Wanafunzi wenye sifa wakosa nafasi vyuo vya Ualimu vya Serikali .

Read Next

Utafiti, watu waliopona Ebola wasumbuliwa na Figo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!