Wanafunzi wenye sifa wakosa nafasi vyuo vya Ualimu vya Serikali .

Wanafunzi 5,252 sawa na asilimia 75% kati ya 7,025 waliokamilisha maombi ya udahili wa kujiunga na vyuo vya ualimu vya serikali wamebainika kuwa na sifa huku wanafunzi 1,773 sawa na asilimia 25% wakikosa sifa za kujiunga na mafunzo hayo.

Taarifa iliyotolewa kwa wanahabari jijini Dodoma na katibu mkuu wizara ya elimu, sayansi na Teknolojia Dkt. LEONARD AKWILAPO imeeleza kuwa kati ya wanafunzi hao waliobainika kuwa na sifa wanafunzi waliopata nafasi ni 2834.

Kwa mwaka wa masomo 2019/2020 wizara ilitangaza nafasi za masomo kupitia Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi NACTE ngazi ya Astashahada na Stashahada za ualimu zipatazo 12,859 kwa vyuo vya ualimu vya serikali 35.

Dkt. Akwilapo anaeleza kuwa kati ya nafasi hizo wanafunzi waliokamilisha maombi ni 7,025 ambapo wenye sifa ni 5,252 na waliopata nafasi ni 2834 ambao wataungana na wale walichaguliwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Vilevile Dkt. Akwilapo ameelezea wasiwasi wa wizara juu ya idadi kubwa ya wanafunzi waliokosa nafasi na kuiagiza NACTE kufungua dirisha dogo la udahili kuanzia tarehe 7 hadi 21 Septemba ili kujaza nafasi hizo kwa kozi mbalimbali.

Wakati huohuo Naibu katibu mkuu anayeshugulikia masuala ya elimu Dkt. AVEMARIA SEMAKAFU amesema kwa muda mrefu changamoto ya lugha ya kiingereza kutumika katika elimu ya ufundi imekuwa kikwazo kwa wanafunzi kujiunga na vyuo vya VETA na kuilazimu wizara kuubadili.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Upinzani Uingereza wajadili kuhusu Uchaguzi wa mapema.

Read Next

Utekelezaji wa Mikopo asilimia nne kwa Vijana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!