Ziara ya Rais Dkt. Magufuli Mkoani Rukwa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli amempa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Rukwa, siku nne kutekeleza agizo lililotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, alilolitoa wiki iliyopita wakati alipokuwa akikagua utendaji wa askari polisi katika eneo la Laela ambapo wananchi walimlalamikia kuhusu utendaji mbovu wa askari wa Kituo Kikuu cha Polisi na kuamuru wahamishwe askari wote, agizo ambalo bado halijatekelezwa.

Mhe.Rais ametoa agizo hilo wakati akiwa katika shughuli za uzinduzi wa barabara ya kiwango cha lami ya Tunduma-Sumbawanga iliyokamilika tangu mwaka 2016, ambapo amempa kamanda huyo wa Polisi saa hizo kutokana na kutoridhishwa na utendaji wa kusuasua wa kamanda huyo.

Ama, kuhusu mradi wa maji wa Shilingi bilioni moja uliotarajiwa kujengwa na kukamilika ili kuwapa unafuu wakazi wa eneo la Laela, Mhe.Rais ameagiza kukamatwa mara moja kwa watuhumiwa wawili walioachiwa kwa dhamana kufuatia tukio la kuungua vifaa vya ujenzi wa mradi huo ambapo ametoa muda wa siku saba kuhakikisha mkandarasi huyo anakamatwa na kurejesha fedha za mradi huo ili kazi iendelee.

Katika hatua nyingine,Mhe.Rais ameagiza watumisho wote waliopangwa kufanyakazi katika Halmashauri ya Sumbawanga Vijijini kuhamia mara moja kwenye halmashauri hiyo ambayo Makao Makuu yake ni Laela, ambapo TANROADS wapewa siku tano kuhamia ofisi za Serikali na kuondoka kwenye jengo la kupanga.

Aidha,baadhi ya mawaziri waliongozana na Mhe.Rais katika ziara hiyo walipata fursa ya kuzungumzia miradi inayofanyika ndani ya mkoa wa Rukwa.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

China yatakiwa kumchunguza Joe Biden.

Read Next

Watu 100 wauawa katika Maandamano Nchini Iraq.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!