Mfuko wa Dunia Global Fund.

Mfuko wa Dunia wa Global Fund jumatano umeanzisha jitihada za ukusanyaji wa Dola Bilioni 14 za kupambana na maradhi matatu duniani ya malaria, ukimwi na kifua kikuu huku ukikabiliwa na sitofahamu kupata ufadhili kutoka kwa wafadhili.

Kwa mujibu wa mashirika yasiyo ya kiserikali NGO’s huenda kiasi hicho cha fedha kikahitajika zaidi kufikia dola bilioni 18.

Mfuko huo unahitaji dola bilioni $14, kiasi ambacho wanasema kitasaidia kuokoa maisha ya watu milioni kumi na sita, na kupunguza maambukizi ya magonjwa hayo milioni 234 na kuiweka dunia kufikia malengo ya umoja wa mataifa ya kumaliza magonjwa ya UKIMWI, Malaria na kifua kikuu ndani ya miaka kumi.

Shirika la afya la umoja wa mataifa (WHO) limesema watu 770,000 wamekufa kutokana na magonjwa nyemelezi yatokanayo na athari za virusi vya UKIMWI, huku kifua kikuuu kikiwa na uwezekano mkubwa kuwapata watu wenye walioathirika na virusi vya UKIMWI, ambapo umegharimu watu takribani milioni 1.7 mwaka 2017 na malaria zaidi ya watu 430,000.

Mkutano huu ni wa sita katika kukuza mfuko huo tangu mwaka 2002, ukiwa na wafadhili wakuu wa mfuko huo, ambapo kwa mujibu wa mkutano huo asilimia 72 ya fedha zilizotumika tangu mwaka 2016 zilipelekwa Afrika na asilimia 20 ilitumika Asia na eneo la Pacific.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Jeshi la Polisi Tarime RORYA lawashikilia watano.

Read Next

Waziri Mkuu azindua Mradi wa Kitalu Nyumba kwa Vijana kwa Nchi nzima.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!