Onyo la CCM kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Makamu mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Philip Mangulla ameonya kwamba Chama hakitasita kufuta uchaguzi wa serikali za mitaa endapo kitapokea malalamiko na kujiridhisha kwamba viongozi waliopata nafasi ya kusimama kwenye uchaguzi huo hakufuata utaratibu wakati wa mchakato.

Mangulla ameyasema hayo nyumbani kwake jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumzia mambo mbalimbali kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo amewataka wale wote wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo kuhakikisha wanafuata maadili kwani ndio nguzo muhimu itakayowezesha kupatikana kwa viongozi bora na wenye sifa.

Akizungumzia umuhimu wa kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura Dkt.Mangula amesema wananchi watumie fursa hiyo vizuri ili waweze kuchagua viongozi wanaowataka huku akikosoa viongozi waliokuwa hawaitishi mikutano na wananchi wao na kwamba hawatoshi kwenye nafasi hizo.

Aidha amewakumbusha wenye nia ya kugombea uongozi katika ngazi mbalimbali kwamba nafasi hizo ni za kujitolea kuwatumikia wananchi wala sio biashara.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Waziri Mkuu azindua Mradi wa Kitalu Nyumba kwa Vijana kwa Nchi nzima.

Read Next

Mkuu wa Mkoa awatembelea Wahanga wa Mafuriko Korogwe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!