Waziri Mkuu azindua Mradi wa Kitalu Nyumba kwa Vijana kwa Nchi nzima.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya tano imeamua kupambana na ukosefu wa ajira kwa vijana kwa kuanzisha programu za kuongeza na kurasimisha ujuzi.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo wakati akizindua mradi wa kitaifa wa mafunzo ya ujenzi na kilimo cha kisasa kwa kutumia teknolojia ya kitalu nyumba (greenhouse) kwenye viwanja vya maonesho vya Ngongo, mjini Lindi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya vijana kitaifa kwa mwaka 2019.

Amesema Mwelekeo wa Serikali hivi sasa ni kuendeleza viwanda na viwanda hivyo vinahitaji malighafi inayotokana na mazao kwa lengo la kuwafanya vijana waweze kuajiriwa kwenye sekta hiyo ya uzalishaji.

Akifafanua kuhusu teknolojia ya kitalunyumba, Waziri Mkuu alisema: ìProgramu hii inasimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na kwamba Serikali inayoongozwa Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli imeweka sisitizo kwenye kilimo hivyo akawataka vijana kuacha dhana kwamba ajira ni ya kushika kalamu na kukaa ofisini.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na wananchi waliohudhuria uzinduzi huo, Waziri wa Nchi OWM – Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Bi. Jenista Mhagama alisema Serikali ilifanya utafiti na kubaini kwamba asilimia 56 ya nguvukazi nchini ni vijana lakini wanakabiliwa na changamoto ya kukosa ajira, huku baadhi ya wadau wakieleza michango ya taasisi zao.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Mfuko wa Dunia Global Fund.

Read Next

Onyo la CCM kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!