Viongozi watatu wasaka suluhisho kuhusu Libya.

Msemaji wa Serikali ya Ujerumani amesema Kansela Angela Merkel amezungumza na viongozi wenzake wa Uturuki na Urusi kuhusu juhudi za kupata suluhisho la kidiplomasia kwa ajili ya Libya.

Kansela Merkel alizungumza jana mara mbili kwa njia ya simu na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na Rais wa Urusi Vladmir Putin juu ya kutafuta suluhisho la mgogoro huo wa muda mrefu.

Katika mazungumzo hayo makubaliano kadhaa yalifikiwa kuimarisha juhudi za kidiplomasia na kwamba walijadiliana kuhusu maendeleo ya Syria.

Kwa upande wake Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki ameonya kuwa mzozo wa Libya unahatarisha nchi hiyo kutumbukia kwenye machafuko na kuwa kama Syria wakati wakijaribu kuharakisha sheria itakayoiruhusu Uturuki kupeleka wanajeshi wake kaskazini mwa Libya.

Wakati huo huo, Ufaransa na Misri zimetoa wito kwa pande zote nchini Libya kujizuia pamoja na maafisa wa kimataifa kuepuka kuuongeza mzozo huo wa Libya.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Wahamiaji haramu tisa kutoka Ethiopia wakamatwa Tanga.

Read Next

Salam za Mwaka Mpya 2020 kutoka kwa Rais wa China Xi Jinping.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!