Maazimio ya Kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi.

Kamati kuu ya halmashauri kuu ya Taifa CCM iliyoketi leo Jijini Dar es Salaam chini ya mwenyekiti wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt. John Pombe Magufuli amepokea taarifa ya awali juu ya utekelezaji kuhusu kuwaita na kuwahoji wanachama watatu ambao ni Mzee Kinana, January Makamba na Ndugu Benard Membe ambao wote walishafika mbele ya kamati ndogo ya udhibiti na nidhamu inayoongozwa na Mzee Philip Mangula.

Akizungumza na waandishi wa habari Katibu wa itikadi na uwenezi wa chama hicho ndugu Hamphrey Polepole amesema, Kamati kuu hiyo imetoa siku saba kwa kamati ndogo ya udhibiti na nidhamu chini ya Mzee Philip Mangula kukamilisha taarifa inayowahusu wanachama hao watatu na baadaye kutakiwa kuiwasilisha katika vikao husika.

Katibu huyo mwenezi wa chama hicho pia amesema kwamba kikai hicho pia kilijadili maandalizi ya mwelekeo wa sera za chama kwa mwaka 2020, maombi ya kujiunga na Chama cha Mapinduzi kwa aliyewahi kuwa Waziri mkuu wa Zamani Ndugu Fredrick Sumaye ambapo Kamati kuu imeelezea kupokea maombi hayo na kwamba kamati hiyo imetaka utaratibu ufuatwe.

Wakati huo huo katika mkutano huo na waandishi wa habari Katibu mkuu wa chama chama CCM Dkt. Bashiru Ally alitoa wasaa wa kuwatangaza madiwani watano kutoka chama cha ACT wazalendo ambao kwa hiyari yao wameamua kujiunga na chama cha Mapinduzi. Madiwahi hao ambao wote ni kutoka katika Halmashauri ya manispaa ya Kigoma ni pamoja na Ndug. Khamis Rashid Khamis Diwani kata ya Gungu, Ismail Hussein-Diwani kata ya Kagera, Hamduni Nassor -Diwani kata ya Kasinirima, Musa Jumanne Ngongolwa- Diwani kata ya Kamampa, na Faud Nassor – Diwani kata ya Kasimbu.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Idadi ya waliofariki kwa mafuriko Iringa yaongezeka.

Read Next

Maziko ya Daniel Arap Moi, Maelfu ya raia wamiminika Kabarak.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!