Maziko ya Daniel Arap Moi, Maelfu ya raia wamiminika Kabarak.

Rais Uhuru Kenyata wa Kenya ameongoza mamia ya watu kushiriki maziko ya rais mstaafu wa awamu ya pili wa Kenya, Daniel Arap Moi yaliyofanyika leo mchana.

Rais Kenyatta amesema kwa upande wake anamuaga mtu aliyemtaja kama baba yake, ambapo Moi alimlea akiwa mwalimu, mshauri wake mkuu na amejifunza siasa kutoka kwake.

Naye Naibu wa rais Kenya, William Ruto amesema licha ya kwamba Moi hakuwazaa yeye na viongozi wengine waliofanikiwa kisiasa kutokana na ulezi wa rais huyo mstaafu, anamshukuru kiongozi kwa manufaa ya uongozi aliyowaletea Wakenya.

Hayati Daniel arap Moi, rais wa zamani wa kenya katika awamu ya pili amezikwa leo kwenye mji wa nyumbani kwake wa Kabarak, Nakuru baada ya maelfu ya watu kutoka ndani na nje ya Kenya kushiriki jana ibada ya kutoa salamu za mwisho mjini Nairobi.

Moi aliyeiongoza Kenya tangu mwaka 1978 hadi 2002 alifariki wiki iliyopita akiwa na umri wa mika 95.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Maazimio ya Kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi.

Read Next

Wafugaji Itilima wafikisha kilio kwa Waziri Mpina.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!