Mfahamu Mtakatifu Valentine, mhubiri wa kikristo.

Leo ni Febuary 14, 2020 watu wengi duniani hufanya maadhimisho ya siku hii kama siku ya Valentine kwa kimombo “Valentine Day”.

Asili ya siku ya wapendanao “Valentine’s Day” ni Mtakatifu Valentine, mhubiri wa kikristo aliyekuwa akiishi karibu na mji wa Roma katika karne ya tatu wakati wa utawala wa Kaisari (Cheo cha Mfalme mkuu kipindi cha utawala wa warumi) Claudis II.

Kaisari Claudis alitaka awe na jeshi kubwa akategemea vijana wangejitolea na kujiunga na jeshi lake. Lakini vijana wengi hawakupenda vita kwakuwa hawakutaka kuziacha familia zao na watoto wao. Claudis akafikiria akaona hawa vijana kuwakomesha waingie jeshini ni kupiga marufuku watu kuoana. Kuanzia hapo akapiga marufuku watu kuoana akitegemea vijana hawatajali sasa kujiunga na jeshi kwa sababu ya familia zao.

Padre Valentinus alipinga jambo hili na hivyo kuendelea kufungisha ndoa kwa siri kwenye makatakombe (mahandaki chini ya kanisa ambako kuna sehemu za ibada kwa watu wachache), alifanya hivyo kwa vile kufunga ndoa hadharani ilikuwa ni kukiuka amri ya wakuu wa dola ya kirumi.

Baadhi ya watu walifichua siri hiyo, na baada ya Mfalme Claudius kupata habari hizi aliamuru Valentinus akamatwe na kuhukumiwa adhabu ya kifo cha kunyongwa, kama shahidi mfia dini kwa ajili ya kutetea waumini wake wafunge ndoa ili waache maisha ya ngono zembe

Wakati akiwa jela akisubiri siku yake ya kunyongwa Valentine alikuwa akitembelewa na vijana waliokuwa wakimpelekea maua kuonyesha wako pamoja nae.

Mmoja wa vijana waliokuwa wakienda kumtembelea ni mtoto wa mkuu wa gereza aliyeitwa Asterius ambaye aliruhusiwa kuingia mpaka kwenye selo la Valentine “kupiga naye stori“.

Kadri siku zilivyokuwa vinasonga mbele Valentine aliangukia katika mapenzi na Asterius, Mtoto huyo wa mkuu wa gereza alilokuwa amefungwa

Akiwa anaendelea kusubiri siku yake ya kunyongwa, Asterius, alipatwa na maradhi ya ajabu ambayo yalisababisha akaribie kukata roho.

Padre Valentine aliposikia habari hizo, aliomba kwenda kuonana naye ambapo alimponya maradhi yaliyokuwa yanamsumbua. Habari za tukio hilo la kipekee, lililodhihirisha upendo wa dhati, zilisambaa kwa kasi ndani na nje ya gereza

Siku chache kabla Padre Valentine hajanyongwa, alimuandikia barua ya kumuaga binti Asterius, chini kabisa akaandika maneno ‘Your Valentine’, akaambatanisha na ua waridi jekundu.
Valentine alinyongwa hadi kufariki dunia tarehe 14 februari mwaka 269 AD. Wafuasi wake waliokuwa wakiyakubali mafundisho yake, waliendelea kuiadhimisha siku hiyo kwa kupeana kadi na barua zenye maneno ‘Your Valentine’ au ‘To My Valentine’ kudhihirisha upendo waliokuwa nao kwa wahusika.

Toka hapo Valentine anakumbukwa kama mtetezi wa wapendanao na sikukuu yake kuadhimishwa Febuari 14 kote duniani.

KUENEA KWAKE DUNIANI:

Kwa kirumi ni siku ya kumbukumbu (memoria day) na sehemu nyingine ni (festum) maana yake sikukuu ya daraja la kwanza kwa kumkumbuka Padri Valentine aliyeuawa na utawala wa kirumi sababu ya kutetea waumini wake kufunga ndoa badala ya kuishi na vimada tu.

Lakini sikukuu hiyo ikaenea sana katika nchi za magharibi na baadaye karibia sehemu kubwa ya ulimwengu na kuisherehekea kama siku ya wapendanao kinyume cha dhamira ya Mtakatifu Valentine. Nchini Marekani Kadi Zaidi ya milioni 190 hutumika kwa wapendanao kutumiana na zinagharimu Zaidi ya Dolla bilioni 18.

Uingereza nao hawako nyuma, nusu ya raia wan chi hiyo hutumia kiasi kikubwa cha pesa katika maandalizi ya siku hii ambapo takwimu zinaonyesha kwamba mwaka 2019 paund bilioni 1.3 zilitumika kusherehekea siku ya wapendanao maarufu “Valentine Day

Nchini Tanzania pia siku hii ya leo inaadhimishwa na baadhi ya watu haswa vijana katika kuonyesha upendo kwa watu wanaowapenda. Maeneo mbalimbali ya burudani na starehe utakutana na mapambo yenye rangi nyekundu yakiwa yamenakishiwa na maua rose kuonyesha mandhari ya wapendanao. Mjini pia utakutana na mapambo yenye rangi nyekundu na nyeusi bila kusahau kadi zenye jumbe mbalimbali zilizoandikwa mashairi ya kimahaba ambazo hutumika kufikisha ujumbe kwa wale wapendanao.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Idadi ya vifo vya Corona yapanda kwa kasi China.

Read Next

Upanuzi wa Chanzo cha Maji, Kata ya Ikwiriri (W) Rufiji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!