Marekani yatangaza hali ya maafa makubwa.

Kufuatia kushamiri kwa mgogoro wa virusi vya Corona nchini Marekani, kwa mara ya kwanza katika ya historia ya nchi hiyo kumetangazwa hali ya maafa makubwa.

Tangazo hilo limetolewa siku ambayo serikali ya Washington imetangaza kuwa idadi ya watu waliopoteza maisha kwa virusi vya Corona nchini Marekani imezidi ile ya Italia na hivyo kuifanya nchi hiyo kushika nafasi ya kwanza duniani.

Jana Rais Donald Trump aliandika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter ambapo sambamba na tangazo hilo katika majimbo yote ya nchi hiyo, alielezea matumaini kuwa Marekani itaibuka mshindi katika vita vya Corona.

Hadi sasa Marekani ina waathirika laki tano na elfu 60 na 433 wa virusi vya corona na watu elfu 22,115 wamepoteza maisha kutokana na virusi hivyo.

Katika hatua nyingine Uchina imeripoti idadi kubwa zaidi ya kesi mpya za coronavirus 108 katika ya wiki sita kwani maambukizo kote ulimwenguni yanazidi milioni 1.8.

Ulimwenguni kote, zaidi ya watu 114,000 wamekufa kutokana na ugonjwa huo , wakati karibu watu 434,000 wamepona, kulingana na data ya Chuo Kikuu cha Johns Hopkins.

Wakati huo huo Urusi pamoja na mataifa yanayozalisha mafuta kwa wingi duniani -OPEC yamekubaliana kupunguza kiwango cha uzalishaji mafuta takribani mapipa milioni 10 kwa siku ili kuidhibiti bei iliyoporomoka kutokana na janga la kirusi cha corona na vita.

Punguzo hilo, ambalo liliafikiwa kwenye mkutano wa wa mataifa hayo ni sawa na asilimia 10 ya kiwango cha kawaida, ingawa katika uhalisia linaweza kufikia hadi asilimia 20.

Mazungumzo ya awali juu ya uzalishaji wa mafuta duniani yalikuwa yamekwama kutokana na mzozo na Mexico, lakini ufumbuzi ulipatikana baada ya mataifa wanachama wa OPEC kuliruhusu taifa hilo la Amerika Kusini kupunguza mapipa 100,000 tu kwa mwezi.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Tahadhari ya Corona kwenye vituo vya Yatima.

Read Next

Nyumba zazingirwa na maji Dsm.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!