Agizo la kufunguliwa Shule na Vyuo laendelea.

Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa amesema agizo la kufungwa kwa shule za awali, msingi, sekondari na vyuo vyote vya elimu ya kati na vya elimu ya juu litaendelea kubaki vile vile hadi hapo Serikali itakapotoa tamko jingine.

Waziri Mkuu ameyasema hayo katika kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Uratibu wa Mapambano Dhidi ya ugonjwa wa Homa ya Mapafu unaotokana na maambukizi ya Virusi vya Corona (COVID-19) ambapo amesema mpaka sasa nchini kuna jumla ya watu 53 waliobainika kuwa na virusi vya corona ikiwa ni ongezeko la wagonjwa wanne ambao wote wapo jijini Dar es Salaam.

Pia, Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesitisha maadhimisho ya Sherehe za Muungano (Aprili 26) pamoja na Sikukuu ya Wafanyakazi (Mei Mosi) ili kuepuka msongamano na kuendelea kuzuia virusi vya corona visisambae zaidi.

Amesema Serikali bado haijatangaza kuhusu kufunguliwa kwa shule, vyuo na shughuli za michezo pamoja na misongamano isiyokuwa ya lazima, hivyo maeneo hayo yataendelea kusalia katika karantini na wanafunzi wote wandelee kubakia majumbani kwao.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. Magufuli ameagiza sh. milioni 500 ambazo zilitengwa kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 56 ya Sherehe za Muungano zipelekwe kwenye mfuko wa kupambana na COVID-19 wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Pia, Waziri Mkuu amewaomba wadau mbalimbali waendelee kuiunga mkono Serikali katika mapambano dhidi ya virusi vya corona kwani janga hilo ni kubwa na wanaweza kutuma fedha kupitia akaunti Na: 9921159801 yenye jina la National Relief Fund Electronic.

Waziri Mkuu ameagiza kuwa wataalamu wanaosimamia utoaji wa huduma katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya wa watu wenye maambukizi ya COVID-19, wakiwemo madaktari wote wapewe vifaa vya kijikinga ili kuhakikisha hawapati maambukizi ya ugonjwa huo.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

India yaongeza muda wa zuio la kutotoka majumbani.

Read Next

Waziri Mkuu apokea Tsh. milioni 500 kukabili corona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!