Kenya imesema Tanzania ni ndugu, miamba ya Uchumi Afrika Mashariki.

Serikali ya Kenya imesema nchi hiyo na Tanzania sio tu ni majirani bali ni ndugu na kwamba changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikijitokeza kwenye mipaka ya nchi hizo kwa siku za karibuni zimesababishwa na mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19, hivyo zisiwe chanzo cha kuvunja udugu huo, bali iwe fursa ya kukaa pamoja na kutafakari namna gani ya kuinua uchumi ambao umetetereka kutokana na janga hilo.

Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Dan Kazungu akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam ameweka wazi kuwa ameagizwa na Rais Uhuru Kenyata kueleza kwamba anaitazama Tanzania kama nchi jirani na ndugu kutokana na urafiki wa muda mrefu lakini pia ushirikiano mzuri wa kibiashara uliopo unaozifanya nchi hizo kuwa miamba ya uchumi katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Balozi Kazungu ametoa ufafanuzi kuhusu mwenendo wa kukabiliana na maambukizi ya Virusi vya Corona kwenye maeneo ya mipaka akisema Kenya haijazuia madereva wanaosafirisha mizigo kuingia nchini humo, bali utaratibu uliowekwa ni kwamba kila dereva anaeingia na kutoka nchini humo ni lazima apimwe iwapo ana maambukizi ya virusi vya Corona.

Balozi huyo wa Kenya nchini Tanzania amesema ni vyema wananchi wa pande zote mbili kuwa na subira hasa wakati huu ambao Mataifa mengi duniani yakitafuta njia bora za kukabiliana na virusi vya Corona.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Juhudi za umoja wa Ulaya kukwamua uchumi wake.

Read Next

Waziri Mkuu awasimamisha kazi watumishi watatu TEMESA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!