Wananchi wamehimizwa kuendelea na tabia ya kunawa mikono, hata pale ugonjwa wa Covid 19 utakapotoweka, kwa kuwa tabia hiyo imesaidia sana kujikinga na magonjwa mengine, mbali ya virusi vya corona.
Wito huo umetolewa jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo, wakati alipozindua mfumo wa kunawa mikono uliojengwa na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira DUWASA, katika soko la majengo.
Kwa upande Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA Eng. David Palangyo ameweka wazi shilingi milioni 5.6 walizozitumia kwa vifaa, huku wakishikiana na Halmashauri ya Jiji la Dodoma kukabiliana na Ugonjwa wa Covid 19.