Rais Dkt. Magufuli atangaza vyuo vyote kufunguliwa Juni Mosi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli ametangaza kufunguliwa kwa Vyuo Vyote nchini tarehe Moja Juni mwaka huu pamoja na kuruhusu Wanafunzi wa kidato sita kurudi shuleni kwa ajili ya kujiandaa na Mitihani baada ya kujiridhisha na kupungua kwa maambukizi ya Corona yanayosababisha Ugonjwa wa Covid-19 hapa nchini.

Mhe .Rais Magufuli ametangaza hayo Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma katika hafla ya kuwaapisha Viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni ambapo i amezitaka Wizara zenye dhamana pamoja na Bodi ya Mikopo Tanzania kuhakikisha ndani ya siku tisa kabla ya kufunguliwa Vyuo wawe wameaandaa utaratibu maalum wa kutoa mikopo kwa wanafunzi wa Vyuo.

Aidha katika Hafla hiyo Mhe Rais Magufuli ameitaka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto pamoja na Watendaji wengine kuhakikisha vifaa mbalimbali vya kujikinga na Corona vinavyotolewa kama msaada vichunguzwe kabla ya kuanza kuvitumia huku pia akiwataka Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa Covid-19 kwani licha ya kupungua kwa maambukizi Ugonjwa bado upo.

Awali Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi,Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi Ummy Mwalimu pamoja na Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo walizungumzia mambo mbalimbali kuhusiana na Viongozi hao wapya walioapishwa.

Viongozi walioapishwa leo ni pamoja na Dkt Godwin Aloyce Mollel Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Balozi wa Tanzania nchini Algeria Jacob Gideon Kingu, Balozi Faustine Martin Kasike anayekwenda Msumbiji, Balozi John Stephen Simbachawene anayekwenda nchini Kenya, John Julius Mbungo Mkurugenzi Mkuu TAKUKURU pamoja na Dkt. Delphine Magere Katibu Tawala Mkoa wa Pwani

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Soko la Mabibo Corona Basi, lanufaika kutengenezewa Vizimba.

Read Next

Nzige, Covid-19 na mafuriko kitisho kwa baadhi ya Nchi za Afrika Mashariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!