Nzige, Covid-19 na mafuriko kitisho kwa baadhi ya Nchi za Afrika Mashariki.

Maafisa wa Benki ya Dunia wanaonya kwamba nzige, COVID-19 na mafuriko ni majanga matatu yanayotishia maisha ya mamilioni ya watu katika baadhi ya mataifa ya eneo la Afrika Mashariki.

Benki hiyo imetenga dola milioni 500 kwa ajili ya nchi zilizoathirika na janga la nzige hao wa jangwani.

Wimbi jipya na kubwa zaidi la wadudu hao waharibifu wa mimea linahofiwa kuvamia mataifa kadhaa ya Afrika Mashariki ambayo hayakuwahi kushuhudia idadi kubwa ya wadudu hao kwa miaka 70 iliyopita. Aidha Mabadiliko ya tabianchi yanatajwa kuwa ni mojawapo ya sababu za kujitokeza kwa wadudu hao.

Umoja wa Mataifa umeonya kwamba uvamizi wa nzige kwa sasa ni mbaya zaidi nchini Kenya, Somalia na Ethiopia.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Rais Dkt. Magufuli atangaza vyuo vyote kufunguliwa Juni Mosi.

Read Next

Ndege ya Ethiopia yasafirisha samaki kutoka Mwanza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!