Dkt. Kigwangala azindua Video kuhamasisha Utalii.

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Khamis Kigwangala amezindua video ya utalii iliyopewa jina la Tanzania Unforgetable yenye lengo la kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini ili kutoa fursa kwa wageni na wenyeji kuvitambua na kuvitembelea vivutio hivyo.

Akizundia Video hiyo Jijini Dar es Salaam Dkt. Kigwangala amesema kuwa video hiyo ya vivutio vya utalii itaitambulisha rasmi Tanzania katika sekta ya utalii kimataifa hivyo kutanua wigo kwa wageni na wenyeji kutambua fursa zilizopo nchini pamoja na kuwavutia kuja nchini kuvitembelea hali ambayo itachangia kukuza uchumi wa nchi.

Licha ya janga la virusi vya Corona, Dkt, Kingwala amesema wameamua kufungua shughuli za utalii nchini lakini kwa kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wataalam wa afya ambapo sekta hiyo tayari imeandaa muongozo husika katika kukabiliana na janga hilo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi mwendeshaji wa bodi ya Utalii Devotha Mdachi amesema video hiyo imetafsiriwa kwa lugha mbalimbali na pia itatangazwa kupitia mitandao ya kijamii, Balozi za Tanzania Nje ya nchi pamoja na vyombo mbalimbali vya habari.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Marekani yatakiwa kuzuia mauaji ya weusi.

Read Next

Kesi ya Uchochezi, Zitto Kabwe atiwa hatiani na kuhukumiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!