Jeshi la polisi Mkoani Mbeya kwa kushirikiana na Jeshi la polisi katika Mikoa ya Songwe Rukwa na Katavi wamewakamata watu 87 wanaotuhumiwa kwa makosa ya mauaji wakiwemo waganga wa kienyeji wanaopiga ramli chonganishi.
Kwa Mujibu wa Taarifa ambayo imetolewa na Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la polisi Ulrich Matei anasema mikoa hiyo imeanza msako maalumu wa kupambana na mauaji yanayotokea katika ukanda huo, hii yote inalenga kukomesha vitendo hivyo.
Aidha kamanda Matei anasema Jeshi la polisi pia linamshikilia mfanyabiashara pamoja na mganga wa jadi wote wakazi wa Jijini Mbeya kwa tuhuma za mauaji , lakini pia akakemea tabia ya vitendo vya kishirikiana.
Aidha jeshi la Polisi limekamata pikipiki zinazodaiwa kuwa za wizi , pombe haramu ya moshi, na bangi.