CCM yawaonya wanachama wanaofanya kampeni za chini chini kabla ya muda.

Chama cha Mapinduzi Cha CCM kimetoa onyo kali kwa wanachama wao ambao wamenza kampeni za Chini chini kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kikisema kuwa kitawachukulia hatua kali wale ambao watabainika.

Onyo hilo limetolewa na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa Bwana Humphrey Polepole wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ofisi ndogo za CCM Lumumba Jijini Dar es Salaam.

Amesema mwanachma yoyote anatakiwa kufuata kanuni ya Chama inayosema hadi pale mwenyekiti wa Chama, ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli atakapotangaza kuanza kampeni za uchagzui wa viongozi mbalimbali.

Aidha amekemea suala zima la rushwa katika chaguzi zote na kuwataka wanachama kutoa taarifa pindi wakibaini kuna dalili ya rushwa inafanywa na mwanachama mwenzao anayetaka madaraka.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

TBC yalipa fidia wananchi eneo la Ujenzi wa Makao Makuu yake.

Read Next

CCM yawaonya wanachama wanaofanya kampeni za chini chini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!