TPA yatoa msaada wenye thamani ya tsh milioni 120.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul makonda amepokea masaada wa vifaa tiba pamoja vifaa vya ujenzi kwa ajili ya sekta ya elimu vyenye thamani ya shilingi milioni 120 kutoka mamlaka ya bandari Tanzania TPA ambavyo imetoa kwa lengo la kurudisha sehemu ya kipato chake kwa jamii.

Akizungumza kabla ya kukabidhiwa vifaa hivyo Makonda amesema vifaa tiba ambavyo ni Ultra-Sound vitapelekwa manispaa ya kigamboni kwa ajili ya kutumika katika hospitali mpya ambayo ujenzi wake umekamilika lakini ilikuwa inakabiliwa changamoto na uhaba wa vifaa pamoja na watumishi huku vifaa vifaa vya vikielekezwa kwenye ujenzi wa ofisi za walimu.

Katika hatua nyingine Bwana Makonda amewataka madereva na makondakta kuacha mara moja kuwanyanyasa wanafunzi wanaokwenda shule katika kipindi hiki kwa kuwaacha vituoni kwa kisingizio cha level seat na kuwataka kuchukua wanafunzi wanne hadi watano ambao wataweza kusimama kwa kuachiana nafasi na kutoa onyo kwa watu waliojitokeza kuanzia jana kukamata bajaj na bodaboda zinazoingia katika ya jiji.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

TAKUKURU yamshikilia Mtendaji Mkuu wa zamani wa MSD.

Read Next

Askari muelimishaji jamii azawadiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!