Zaidi ya watu 20 wauwawa katika shambulio huko nchini Mali.

Watu Ishirini na sita wameuawa katika shambulio katika kijiji kilicho kati mwa Mali,ambapo maafisa wasema tukio limejiri katika ghasia za hivi karibuni kugonga Taifa hilo lililopo Afrika Magharibi.

Aly Barry ni afisa kutoka Tabital Pulaaku katika Shirika la Fulani nchini Mali,ameongeza kuwa Shambulio la June Tano lililenga kijiji cha Fulani huko Binedama katika mkoa wa Mopti, alisema

Maafisa wengine wawili wa eneo hilo wamethibitisha kutokea kwa Shambulio hilo.

Huko Leo ikiwa ndio Siku ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu na Wakenya karibu wote ya kusitisha hatua ya ya kutotoka nje kuanzia saa moja usiku hadi kumi na moja asubuhi inafikia ukomo wake baada ya kuongeza kwa siku 21 zaidi mwezi uliopita.

Hatua hii iliwekwa kama njia moja ya kukabiliana na virusi vya corona nchini humo.

Hata hivyo, baadhi ya maafisa waandamizi serikalini wamekuwa wakijaribu kupunguza matarajio ya Wakenya kwa kuonyesha kwamba kuna uwezekano kusiwe na tofauti kubwa hasa baada ya nchi hiyo kushuhudia ongezeko la juu la idadi ya wanaoambukizwa virusi vya corona kila uchao.

Baadhi ya mashirika ya Kidini yamemuandikia Rais rasmi yakitoa wito wa kupitiwa tena kwa hatua hiyo na kuahidi kwamba iwapo ibada zitaruhusiwa kuanza tena watahakikisha miongozo iliyotolewa na wizara ya afya inatekelezwa kwa ukamilifu.

Na huko Nchni Nigeria imeanza kuondoa zuio na kulegeza sheria kali zilizokuwa zimewekwa kwa ajili ya kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa Covid-19 ulioua mamia ya watu nchi humo.

Kwa mara kwanza baada ya wiki kumi, waumini wa Kiislamu katika mji mkuu Abuja jana walishiriki Sala ya Ijumaa katika misikiti mbalimbali ya jiji hilo,ambapo Waumini walipimwa kiwango cha joto la mwili kabla ya kuruhusiwa kuingia misikitini, huku wakilazimika kuchunga sheria ya kutogusana.

Hata hivyo shule na viwanja vya ndege vimeendelea kufungwa nchini humo,tangu lilipoanza wimbi la maambukizi ya corona hadi hivi sasa, Nigeria imeweka sheria kali za kukabiliana na ugonjwa huo ulioenea dunia nzima.

Hadi kufikia sasa, nchi hiyo ya Magharibi mwa Afrika ina Kesi 11,500 za watu walioambukizwa ugonjwa hatari wa COVID-19 na watu zaidi ya 300 wameshafariki dunia.

Hivi Karibuni nchini Tunisia pia ilifikia uamuzi wa kufungua mipaka yake ili kuokoa sekta ya utalii,Mipaka ya ardhini, angani na majini ya nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika inatarajiwa kufunguliwa Julai 27.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

TPA yakabidhi JWTZ vichanja vya kubebea mizigo.

Read Next

Polepole atoa ufafanuzi kuhusu viongozi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!