Messi aungana na wachezaji wenzake kufanya mazoezi Barcelona.

Nyota wa Barcelona Lionel Messi jana ameungana na wachezaji wenzake ikiwa ni maandalizi kuelekea mechi yao ya ligi kuu itakayopigwa jumamosi ijayo Juni 13 dhidi ya Timu ya Real Mayoka.

Messi amerejea jana baada ya kukosa mazoezi kwa wiki moja kutokana na maumivu ya mguu yaliyokuwa yanamsumbua, yakimlazimu kukosa sesheni za mazoezi za jumatano na ijumaa, lakini jumamosi iliyopita alifika katika uwanja wa Barcelona kumanya mazoezi binafsi.

Alipoulizwa kuhusu nafasi yake kwenye kikosi kitakachoshuka dimbani dhidi ya Mayoka, Kocha wa Barcelona CHIKE SETIEN, amesema messi pamoja na wachezaji wengine ambao ni majeruhi watatazamwa uimara wa afya zao pindi itakapofika wakati wa mechi.

Ligi kuu ya nchini Hispania LA LIGA inarejea baada ya kusimama kwa miezi mitâtu kutokana na janga la Corona, na hadi wakati huo Barcelona ndiyo walikuwa wanaongoza kwenye msimamo wa ligi kwa kuwa na alama 58 baada ya kucheza mechi 27.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Mshukiwa wa mauaji Marekani awekewa dhamana.

Read Next

Pinda na tathimini ya Uchaguzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!