Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amefariki dunia kutokana na ugonjwa wa moyo baada ya kulazwa jana katika Hopsitali ya Karusi nchini humo.
Marehemu Rais Nkurunziza aliyekuwa na umri wa miaka miaka 55 ameliongoza taifa la Burundi tangu mwaka 2005 na alitarajiwa kukabidhi madaraka Agosti mwaka huu kwa mshirika wake, Rais Mteule Evariste Ndayishimiye ambaye mapema mwezi huu alitangazwa mshindi wa kiti cha urais katika uchaguzi wa kidemokrasia ulioshirikisha vyama vingi Mei mwaka huu.