Dkt. Abbas akagua uwanja wa CCM Mkwakwani.

Katibu mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambae pia ni Msemaji mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas ametembelea na kukagua uwanja wa CCM Mkwakwani kujionea namna maandalizi ya mechi yalivyo katika kufuata taratibu za Serikali za kupambana na Ugonjwa wa Covid 19.

Dkt. Abbas amesema zipo kanuni za msingi za kiafya michezoni ambazo ni lazima zizingatiwe hasa katika uvaaji barakoa.

Hii ni ziara maalum ya Kukagua viwanja vya mpira vitakavyotumika kwaajili ya mechi mbalimbali kama vinatekeleza maelekezo ya serikali katika kujikinga na virusi vya Corona.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Madereva wa mabasi ya abiria walalamika.

Read Next

Diwani wa CHADEMA kata ya Mjimwema ahamia CCM Njombe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!