Malawi yarudia kupiga kura ya Urais.

Malawi leo imerudia uchaguzi wa Rais baada ya Mahakama ya nchi hiyo kuyafuta matokeo ya mwaka 2019 ambayo Rais Peter Mutharika alishinda. Washindani wakuu kwenye uchaguzi huo ni Rais Mutharika na Dkt.Lazarous Chakwera.

Katika uchaguzi mkuu wa Rais nchini humo uliofanyika mwaka uliopita, Rais Peter Mutharika wa chama tawala cha Democratic Progressive, DPP, alimshinda kwa asilimia ndogo, Dkt. Lazarus Chakwera, mgombea anayeungwa mkono na muungano wa vyama vya upinzani, kikiwemo cha Malawi Congress na United Transformation Movement.

Upinzani uliwasilisha kesi katika mahakama ya kikatiba kuyapinga matokeo hayo ukidai uchaguzi huo ulikumbwa na matukio ya udanganyifu,ambapo Mahakama hiyo iliyafuta.

Vuguvugu la kutetea haki za binadamu HRDC, limekuwa likiongoza maandamano kushinikiza mabadiliko nchini Malawi,ambapo kiongozi wa vuguvugu hilo Gift Trapence amesema uchaguzi mpya utawapa nguvu wananchi wa Malawi.

Mwezi Aprili 27 mwaka 2019 Waandamanaji mjini Lilongwe waliopinga ushindi wa Rais Peter Mutharika walidai kuwa matokeo ya uchaguzi huo yalichezewa na haki haikutumika hivyo kutaka uchaguzi huo usitambuliwe.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Tuzo za wanahabari za SADC.

Read Next

Jacob Zuma afikishwa mahakamani tena.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!