Wahamiaji sita wafariki na mwanamke mmoja ajifungua.

Shirika la Uhamiaji la UN limeeleza kuwa Miongoni mwa Wahamiaji 93 waliookolewa mwambao wa Libya mmoja wao amejifungua Baharini huku wengine Sita wamefariki njiani na wale walionusurika walirudishwa katika mji wa bandari wa Khoms, kilomita 120 sawa na Maili 75 Magharibi mwa mji mkuu wa Tripoli.

Taarifa hii ni kutoka Shirika la Kimataifa la Uhamiaji – IOM limeandika kupitia Mtandao wake wa Twitter, kwamba Miongoni mwao alikuwa ni mwanamke aliyejifungua hivyo kupelekea kufanya hatari ya kuvuka Bahari ya Mediterranean.

Libya ilitupwa katika machafuko baada ya mauaji ya Dikteta wa zamani Muammar al- Gaddafi katika ghasia zilizofanywa na NATO mwaka 2011.

Wafanyabiashara mbalimbali walitoa angalizo kuwa machafuko hayo yatapelekea nchi ya Afrika Kaskazini kuwa njia Kuu ya uhamiaji kuelekea Ulaya.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Tanzania kuisaidia Burundi kuwa mwanachama wa SADC.

Read Next

Mkataba wa ujenzi barabara ya Ruangwa – Nanganga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!