Miili 100 yapatikana katika mgodi wa Madini ya Jade.

Zaidi ya miili mia moja imepatikana kutoka katika mgodi mmoja wa madini ya Jade nchini Myanmar kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na mmomonyoko wa udongo katika ajali ambayo inaelezwa kuwa ni mbaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo.

Janga hilo limetokea baada ya mvua kubwa kunyesha kwa muda mfupi na maji na matope kupita katika mgodi huo uliopo katika mpaka wa Myanmar na China ambayo ndio mtumiaji mkubwa wa madini hayo.

Janga hilo limetokea katika Jimbo la Kachin ambako wahusika wanasema wachimbaji walipewa onyo na mamlaka husika kuhusu kunyesha kwa mvua kubwa lakini walipuuza.

Waokoaji wanafanya kazi kwa bidii kuweza kutoa miili hiyo kwenye mgodi na msemaji wa kikosi cha uokoaji,Than Win Aung, amesema kuwa vifo vingekuwa juu zaidi ya vilivyotokea endapo wasingechukua hatua ya kuwaonya wachimbaji hao.

Madini hayo ambayo yanathaminiwa na wananchi wa China yanachimbwa kwa kiasi kikubwa na wachimbaji wadogo ambao hawana vifaa vya kujikinga au kuchimbia.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Lukuvi kutaja majina ya viongozi wanaopora ardhi.

Read Next

Misingi iliyoifikisha Tanzania Uchumi wa Kati.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!