Mkuu wa Mkoa Mpya Njombe aomba ushirikiano kwa Viongozi.

Mkuu mpya wa mkoa wa Njombe Marwa Mwita Rubirya aliyeteuliwa na Rais Dkt. John Magufuli kuchukua nafasi ya aliyekuwa mkuu wa mkoa huo Christopher Ole Sendeka ameripoti katika ofisi za mkuu wa mkoa wa Njombe na kutoa rai kwa viongozi wenzake kutoa ushirikiano kwa ajili ya kusukuma maendeleo ya mkoa huo.

Akipokelewa katika ofisi za mkoa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Katarina Revocati pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri na watumishi wa ofisi ya mkoa, Mheshimiwa Rubirya amesema amewasili mkoani Njombe kwa dhamira moja ya kuwatumikiwa wananchi na kusisitiza ushirikiano kwa viongozi.

Awali Katibu Tawala wa Mkoa wa Njomb, Katarina Revocati akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Njombe amesema makabidhiano rasmi na aliyekuwa mkuu wa mkoa huo Mhe. Ole Sendeka yanaandaliwa.

Nao viongozi wa wilaya ya Njombe akiwemo mkuu wa Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri pamoja na Katibu Tawala wa wilaya hiyo Emannuel George wakatoa neno kwa kiongozi huo wakati wa kumkaribisha mkoani hapa.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Ubalozi mdogo wa China mjini Houston waamuriwa kufungwa na Marekani.

Read Next

Wasimamishwa kupisha Uchunguzi wa TAKUKURU.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!