Wasimamishwa kupisha Uchunguzi wa TAKUKURU.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU imeunda tume huru ya wataalam wanne watakaochunguza thamani ya fedha katika miradi ya ujenzi wa majengo saba ya ofisi za taasisi hiyo yaliyotiliwa shaka na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wakati akizindua ofisi za wilaya ya Chamwino huku ikiwasimamisha kazi watumishi wote tisa walioshiki katika usimamizi wa majengo hayo ili kupisha uchunguzi huo utakaofanyika kwa siku saba.

Ni kauli aliyoitoa Rais Dkt. Magufuli wakati wa uzinduzi wa ofisi za TAKUKURU wilaya ya Chamwino, akieleza kutoridhishwa na thamani ya fedha iliyotumika katika ujenzi wa jengo hili kiasi cha shilingi milioni 143.

Majengo yatakayochunguzwa ni majengo yaliyojengwa katika wilaya za Chamwino,Mpwapwa,Ngorongoro,Manyoni,Masasi,Namtumbo na Ruangwa ili kubaini endapo thamani ya fedha iliyotumika inaendani na majengo hayo.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Mkuu wa Mkoa Mpya Njombe aomba ushirikiano kwa Viongozi.

Read Next

Rais Dkt. Magufuli aongoza kuaga Kitaifa mwili wa Hayati Mzee Mkapa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!