Mzee Mkapa azikwa Kijijini kwake Lupaso Mtwara.

Mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tatu Hayati Benjamini Mkapa umezikwa leo katika kijiji cha Lupaso Wilayani Masasi Mkoani Mtwara.

Akiwahutubia waombolezaji kijijini hapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli amesema Hayati Mkapa alikuwa mzalendo aliyewapenda wananchi wake, hivyo amewataka wananchi kumuombea lakini pia ametumia nafasi hiyo kuishukuru kamati ya maandalizi ya mazishi pamoja na viongozi wa dini kwa kushiriki kikamilifu shughuli ya mazishi.

Rais Magufuli amesema Hayati Benjamini Mkapa aliyaishi maisha yake kwa upendo Mkubwa hivyo amewataka wananchi kumuombea Mama Anna Mkapa pamoja na familia ya mzee Mkapa kwa ujumla ili iendelee kuishi kwa upendo hasa katika kipindi hiki kigumu wanachopitia.

Awali Rais Mstaafu awamu wa nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema Hayati Mkapa alikua msaada mkubwa kiutendaji aliyeuchukia umasikini na ndiye aliyetengeneza dira ya Taifa ya Mwaka 2025 Tanzania kufikia uchumi wa kati Huku Rais Mstaafu awamu ya Pili Ally Hassan Mwinyi akitaka wananchi kumuombea ambapo pia Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dkt Alli Mohamed Shein akisema Kifo cha Mzee Mkapa ni Pengo kubwa kwa kuwa alikuwa na uwezo mkubwa wa kubuni mambo ya maendeleo.

Aidha Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania alisoma salamu za rambirambi zilizotumwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuomboleza msiba huu.

Baada ya mwili wake kupumzishwa kaburini ma kuwekwa mashada ya maua ndipo mizinga 21 ikapigwa.

Hayati Benjamin William Mkapa alizaliwa Novemba 12 mwaka 1938 Mkoani Mtwara, alifanikiwa kushika Nyadhifa mbalimbali za uongozi,ndani na nje ya nchi, na kutoa mchango mkubwa katika masuala mbalimbali kikanda na kimataifa na alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tatu kuanzia mwaka 1995 hadi mwaka 2005 atakumbukwa kwa sera yake ya uwazi na ukweli.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahali pema peponi AMINA.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Rais Dkt. Magufuli aongoza kuaga Kitaifa mwili wa Hayati Mzee Mkapa.

Read Next

Tanzania yachukuwa Uenyekiti wa Nchi za OACPS na kuelezea kipaumbele chake wakati wa Uenyekiti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!