Mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi mikoa ya Dsm na Pwani.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imeanza kutoa Mafunzo ya Siku tatu kwa Wasimamizi wa Uchaguzi katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani huku ikiwataka wasimamizi hao kuhakikisha wanazingatia Katiba, Sheria na Kanuni za Uchaguzi na Kuhakikisha Wanazingatia haki na Wajibu katika Kutekeleza Majukumu yao.

Akifungua Mafunzo hayo jijni Dar es Salaam, Kamishna kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi,Asina Omar amewataka Wasimamizi hao kutoka ngazi za Mikoa pamoja na Majimbo kuhakikisha kuwa taratibu zote za Kikatiba na Kisheria zinafuatwa katika kusimamia Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba Mwaka huu.

Aidha Tume ya Taifa ya Uchaguzi imewataka Wasimamizi hao kuhakikisha wanayatambua Maeneo ya Vituo vya Kupigia kura mapema, kuzingatia Umbali wa Vituo kwa watu wenye Changamoto ya Ulemavu pamoja na kutatua Changamoto kwa haraka pindi zinapojitokeza.

Kabla ya Kuanza kwa Mafunzo hayo Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Kinondoni Jacob Sifa alisimamia Viapo Viwili kwa Wasimamizi hao ikiwemo cha kujivua Kwa Uanachama wa chama cha Siasa wasimamizi hao na cha Utunzaji wa siri wakati wa zoezi la Uchaguzi.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Tanzania yachukuwa Uenyekiti wa Nchi za OACPS na kuelezea kipaumbele chake wakati wa Uenyekiti.

Read Next

Polisi Kigoma wadhibiti vurugu za Wananchi kata ya Mwanga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!