Polisi Kigoma wadhibiti vurugu za Wananchi kata ya Mwanga.

Jeshi la polisi mkoani Kigoma linawashikilia watu saba ambao ni wakazi wa kata ya Mwanga ndani ya Manispaa ya Kigoma ujiji mkoani Kigoma kwa tuhuma za kufanya fujo na uhalibifu wa nyumba pamoja na uporaji wa samani mbalimbali za ndani.

Ilikuwa ni majira mchana katika mtaa wa Yusufu kata ya Mwanga Manispaa ya Kigoma Ujiji ambapo zilizuka vurugu za kutaka kumdhuru mmoja wa wakazi wa mtaa huo na kusababisha taharuki kubwa ambapo jeshi la polisi lilifika katika eneo hilo na kulazimika kutumia mabomu ya machozi na risasi kuwatawanya wananchi.

Kamanda wa polisi mkoani Kigoma James Manyama ameeleza kuwa chanzo cha tukio hilo ni wananchi kumutuhumu Joctan Maganga ambaye ni mwandishi wa habari wa kujitegemea kuhusishwa na tukio la upoteaji wa kijana aliyejulikana kwa jina la Philipo Hussein mwenye umri wa miaka 21.

Ndugu wa kijana huyo ambaye anaelezwa kupotea kwa takribanii siku saba wanaeleza kuwa kulikuwa na mahusiano yasioridhisha baina ya kijana huyo na Jocta Maganga malumbano yaliyodumu kwa zaidi ya mwaka chanzo ikiwa ni ardhi wakigombea mipaka ya katika eneo wanaloishi.

Aidha katika tukio hilo askari wawili wa jeshi la polisi mkoani hapa wamlijeruhiwa wakati wakijaribu kuzuia vurugu na uharabifu wa nyumba na wizi wa dhamani zilizokuwa ndani ya nyumba hiyo.

Katika hatua nyingine jeshi la polisi mkoani hapa limemkamata mtuhumiwa mmoja katika kata ya Kalinzi wilaya ya Kigoma ambaye jina lake limehifadhiwa akiwa na silaha moja aina ya AK-47 ikiwa na magazine moja yenye risasi 30.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi mikoa ya Dsm na Pwani.

Read Next

Ndege ya kwanza Shirika la Ndege Rwanda yatua tena nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!