Ndege ya kwanza Shirika la Ndege Rwanda yatua tena nchini.

Baada ya serikali kufungua safari za anga la Tanzania,hatimaye ndege ya kwanza ya shirika la ndege la Rwanda imeanza safari zake hapa nchini kwa kutua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) na abiria kutoka mataifa mbalimbali.

Akizungumza baada ya kuwasili kwa ndege hiyo meneja shirika la ndege la Rwanda hapa nchini Bw Jimmy Mitali anaeleza faraja yao baada ya kuanza kwa safari hizo.

Kwa upande wake kaimu mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Kadico inayosimamia uwanja wa KIA Christina Mwakatobe ameelezea Ujio wa kuanza safari za ndege ya Rwanda hapa nchini umekuwa ni muhimu sana pamoja na ndege nyingine kutoka nchi za ulaya kwani inaonyesha kuwa nchi ni salama haswa katika ugonjwa wa Covid-19.

Fransice malugu-mwakilishi wa bodi ya utalii TTB, amesema kwa sasa mashirika mbali mbali yaliyo kuwa yamesitisha safari zake kwa sasa yameanza kurejesha tena na kwa utalii ni swala zuri na kuwataka wananchi wote kuendelea na utaratibu wa kujikinga na corona.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Polisi Kigoma wadhibiti vurugu za Wananchi kata ya Mwanga.

Read Next

Mkutano wa SADC wa Katiba na Sheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!