Mlipuko Mkubwa waacha Maafa Lebanon.

Waokoaji nchini Lebanon wanaendelea kufukua vifusi kujaribu kuwatafuta manusura wa milipuko miwili mikubwa kwenye ghala la kemikali iliyoutikisa mji mkuu Beirut, ambapo mpaka sasa taarifa zinaeleza kwamba watu 78 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 4,000 wamejeruhiwa.

Maafisa wa serikali wanasema huenda idadi ya vifo na majeruhi ikaongezeka wakati jitihada za uokozi zikiendelea, huku majumba, miundombinu, magari vikiharibiwa vibaya kutokana na mlipuko huo.

Milipuko hiyo miwili kwa pamoja ilitokea jana jioni kwenye ghala linalohifadhi vitu vinavyolipuka katika bandari ya Beirut inatajwa kuwa mikubwa kabisa kuwahi kutokea kwa miaka kadhaa.

Rais Michel Aoun amesema kwamba tani 2,750 za kemikali ya Ammonium Nitrate, inayotumika kwa ajili ya mbolea na mabomu, zilikuwa zimehifadhiwa kwa miaka sita kwenye bandari hiyo bila ya kuwekewa taratibu za kiusalama, jambo aliloliita halikubaliki.

Tayari Rais huyo ameitisha mkutano wa dharura wa baraza la mawaziri leo ambapo Waziri Mkuu Hassan Diab aliahidi kwamba kutakuwa na uwajibikaji kutokana na milipuko hiyo na kwamba waliohusika “watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Hata hivyo maafisa wa serikali mpaka sasa hawajataja nini hasa chanzo cha mlipuko huo uliochochea moto, lakini chanzo kimoja cha usalama na vyombo vya habari vya Beirut kilisema cheche za moto zilitokana na wafanyakazi wa kuchomelea vyuma waliokuwa wakiziba tundu kwenye ghala hilo.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

CCM yatangaza rasmi mgombea Urais aliyepitishwa.

Read Next

Rais Dkt. Magufuli kuchukua fomu Kesho NEC.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!