Mtandao wa Facebook wamuadhibu Rais Trump.

Mitandao ya kijamii Facebook na Twitter imemuadhibu Rais Donald Trump na kampeni yake kwa kutuma ujumbe ambao mitandao hiyo inadai ni ya kupotosha ambapo Rais huyo alidai watoto ”wanakaribia kuwa na kinga kamili” ya virusi vya corona.

Facebook ilifuta ujumbe huo wa sauti kutoka kwenye mahojiano aliyoyafanya na kituo cha habari cha Fox News – ikisema kuwa ujumbe huo una “ujumbe wenye madhara wa taarifa za kupotosha kuhusu Covid- 19 “.

Baadaye Twitter ilifuatia ikisema kuwa imefunga akaunti ya kampeni ya Rais Trump hadi ujumbe wake wa sauti sawa na huo utakapoondolewa. Washauri wa Marekani wa afya wamesema wazi kuwa watoto hawana kinga kwa virusi vya corona.

Msemaji wa Facebook mapema jana alinukuliwa akisema kuwa video hiyo ina madai ya uongo kwamba watoto wana kinga ya COVID-19 jambo ambalo ni ukiukaji wa sera za mitandao juu ya taarifa potofu zenye madhara kuhusu COVID.”

Ilikua ni mara ya kwanza kwa kampuni hiyo kubwa ya mtandao wa kijamii kuchukua hatua ya kuondoa ujumbe uliotumwa na rais kwa misingi ya sera yake juu ya taarifa potofu kuhusu virusi vya corona, lakini si mara ya kwanza kumuadhibu Bwana Trump kutokana na ujumbe aliotuma kwenye ukurasa wake.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Rais Dkt. Magufuli achukua fomu ya Urais NEC.

Read Next

Tanzania yaokoa Tsh. Bilioni 700 kutibu watu nje ya Nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!