Rais Dkt. Magufuli achukua fomu ya Urais NEC.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na mgombea wa Urais kwa Tiketi ya Chama hicho ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo amechukua fomu ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi Mkuu ujao katika Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi yaliyoko Jijini Dodoma

Mgombe huyo wa CCM aliyeambatana na Mgombea mwenza wa CCM Mama Samia Suluhu Hassa wakisindikizwa na viongozi wengine waandamamizi na wanachama wa CCM aliwasili katika Ofisi za Tume ya Uchguzi NEC iliyoko eneo la Njedengwa jijini Dodoma majira ya Asubuhi ili kutimiza azma aliyopewa na Chama cha Mapinduzi ya kupeperusha Bendera ya Chama hicho katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Akikabidhi Fomu hizo za kugombea Urais kwa Mhe. Magufuli, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Semistocles Kaijage pamoja na mengine ametoa maelezo kuhusu hizo, taratibu na maadili ya Uchaguzi.

Mara baada ya kukabidhwa Fomu hizo Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Mgombea mweza Mama Samia Suluhu Hassan walielekea Makao Makuu ya CCM Dodoma (White House) ambako walizungumza kwa kifupi na Wanachama na wananchi wa Dodoma kuelezea dhamira yao ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuongoza Taifa kwa kipindi cha pili.

Aidha Mhe. Rais Magufuli amesema CCM na wagombea wake wamejipanga kufanya Kampeni za Kistaarabu zisizo za Kibaguzi katika Uchaguzi Mkuu Ujao katika kipindi chote cha kampeni hadi matokeo yatakapotangazwa.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Rais Dkt. Magufuli kuchukua fomu Kesho NEC.

Read Next

Mtandao wa Facebook wamuadhibu Rais Trump.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!