Kilele cha siku ya kitaifa ya lishe.

Watanzania wameungana katika kilele cha Siku Ya Lishe Kitaifa ambapo Waziri Wa Afya, Maendeleo Ya Jamii, Jinsia Wazee Na Watoto Ummy Mwalimu ameagiza kuanzia Septemba Mosi mwaka huu kila shule ya Msingi na Sekondari itoe huduma ya uuzaji wa maziwa kwa gharama nafuu ili kukabiliana na changamoto ya matumizi ya vyakula visivyo na virutubishi kwa wanafunzi vinavyouzwa kiholela mashuleni.

Ni maadhimisho ya siku ya kitaifa ya lishe nchini ambayo yanafanyika kwa mara ya kwanza lengo likiwa ni kuikumbusha jamii juu ya matumizi sahihi ya vyakula vyenye virutubishi.

Aidha waziri Ummy akaeleza makundi ya vyakula yanayotakiwa kupewa kipaumbele kutokana na wengi wa Watanzania kutoyazingatia.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya chakula na lishe nchini Dkt. Germana Leyna akatoa rai taasisi na sekta binafsi mbalimbali kuwekeza katika masuala ya Lishe.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Pato la Taifa kwa mwaka laongezeka.

Read Next

Juhudi za kuwapatia wananchi vyeti vya kuzaliwa mkoani Tanga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!