Serikali imeeleza kuwa pato la Taifa kwa mwaka limeongezeka na kufikia trilioni 124 ikilinganishwa na trilion 52.9 kwa miaka 10 iliyopita kiwango ambacho hakikuwahi kufikiwa tangu nchi ipate uhuru.
Msemaji mkuu wa serikali Dkt. Hassan Abbas ameeleza hayo jijini Dodoma na kubainisha kuwa pato la taifa ni kupimo cha kukua kwa uchumi wa nchi ambapo kwa upande wa pato la mwananchi limeongezeka kutoka laki 9 hadi milion 2 kwa mwaka kwa kipindi cha miaka mitano.
Ameeleza kuwa kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita pato la taifa likikuwa shilingi trillion 52.9.
Kuhusu hali ya mfumuko wa Bei Dkt. Abbas ameeleza kuwa upo katika wastani mzuri ambao ni chini ya asilimia 5 ambao ni wa chini kwa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya SADC.