Vijana wahimizwa kudumisha uzalendo na amani.

Wakati Taifa likielekea kwenye uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo amewataka vijana wanaopatiwa mafunzo ya mgambo kuhakikisha wanadumisha moyo wa uzalendo na kuwa walinzi wa amani kwa kuwafichua wale wote wenye nia ya kuhatarisha amani hiyo.

Mkuu wa Wilaya Jokate Mwegelo amesema vijana wanaopatiwa mafunzo hayo wanatakiwa kutokubali kurubuniwa na wenye nia za kuvuruga amani ya nchi na badala yake wanatakiwa kuwweka kipaumbele katika kulinda amani na utulivu nchini.

Kisha mkuu huyo wa wilaya akaagiza wasichana waliopo katika mafunzo hayo kuhakikisha wanapatiwa taulo za kike ili kuongeza moyo wakiwa mafunzoni.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

JKT wajipanga kuzalisha chakula cha kutosha.

Read Next

Wafanyakazi 16 wa bandari ya Beirut wakamatwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!