Wafanyakazi 16 wa bandari ya Beirut wakamatwa.

Siku mbili baada ya mlipuko mkubwa uliotokea kwenye eneo la Bandari katika mji mkuu wa Lebanon , Beirut wafanyakazi 16 wa bandari hiyo iliyoko Pwani ya bahari ya Mediterania wamekamatwa.

Kwa mujibu wa mwanasheria mkuu wa jeshi la nchi hiyo Faki Akiki, uchunguzi unafanyika dhidi ya maafisa wa bandari pamoja na maafisa wa forodha kuhusiana na mlipuko huo.

Serikali ya Lebanon, ambayo inakabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa wananchi kutokana na kinachoelezwa kuwa ni mdodoro wa kiuchumi ulioikumba nchi hiyo. Aidha Serikali imeahidi kutoa maelezo kamili kuhusiana na chanzo cha mlipuko huo mapema iwezekanavyo.

Wengi wa wananchi wanadai kufanyika kwa uchunguzi wa kimataifa wa tukio hilo . Vikozi vya uokoaji vimekuwa katika juhudi za kuwatafuta watu 100 ambao bado hawajulikani waliko. Kwa mujibu wa Wizara ya Afya nchini humo, idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na mlipuko huo sasa imefikia watu 149.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Vijana wahimizwa kudumisha uzalendo na amani.

Read Next

Pato la Taifa kwa mwaka laongezeka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!