Wakili Mkuu wa Serikali atoa ufafanuzi.

Wakili mkuu wa serikali Gabriel Malata ametolea ufafanuzi juu ya maamuzi ya mahakama ya Rufaa Tanzania katika shauri la rufaa kuhusu kifungu cha 148(5) cha sheria ya mwenendo wa mashauri ya jinai kinachozuia dhamana kwa baadhi ya makosa makubwa.

Makosa hayo ni pamoja na mauaji,uhaini, utakatishaji fedha,usafirishaji uuzaji wa madawa ya kulevya na ugaidi.

Wakili mkuu wa Serikali Malata ametoa ufafanuzi huo baada ya mahakama ya Rufaa Tanzania kutoa uamuzi wa rufaa Na.175/2020 iliyokatwa na serikali baada ya mahakama kuu ya Tanzania kuridhia ombi lililotolewa katika shauri lililofunguliwa na Dickson Paul Sanga katika mahakama hiyo kuu ya Tanzania akidai pamoja na mambo mengine kuwa kifungu cha 148(5) cha sheria ya mwenendo wa mashauri ya jinai sura ya 20 ni batili kwa kuwa kinakiuka katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kwa kuondoa haki ya kupewa dhamana kwa mtu aliyeshtakiwa kwa makosa makubwa.

Mahakama ya Rufaa chini ya jopo la majaji watano baada ya kusikiliza shauri hilo ilikubaliana na mkata rufaa ambaye ni serikali kuwa kifungu hicho sio batili na wala hakikinzani na katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Aidha Wakili mkuu wa serikali alitumia fursa hiyo kuwambusha mawakili kukumbuka viapo vyao kufuatia baadhi yao kutafsiri vinginevyo rufaa hiyo jambo ambalo limeonyesha taswira mbaya ya kuikejeli mahakama.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Tanzania yaokoa Tsh. Bilioni 700 kutibu watu nje ya Nchi.

Read Next

JKT wajipanga kuzalisha chakula cha kutosha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!