Kocha asema timu ya Atalanta itapigana kulinda heshima UEFA.

Naye Kocha mkuu wa timu ya Atalanta, Gian Piero Gasperini amesema klabu yake imeonyesha kuwa mpira wa miguu ni mchezo wa wazi, na kwamba kombe la klabu bingwa ni mali ya kila klabu ya Ulaya, akisisitiza kuwa hata ambazo hazina majina makubwa.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Lisbon kuelekea mechi dhidi ya PSG, amesema anachopigania na timu yake ni kupata ushindi wa kombe la klabu bingwa. Aidha aezungumzia mpangilio wa kikosi, kujituma kwa wachezaji na utayari wa kutaka kupata matokeo mazuri kwenye mechi iliyo mbele yao.

Kama ilivyo kwa PSG, timu ya Atalanta imewasili jana mjini Lisbon na tayari imeendelea kufanya mazoezi ya kujinoa kuwakabili PSG ambao kwa mujibu wa Gasperini ni timu ya daraja la juu. Hata hivyo ameelezea kujivunia uwezo wa wachezaji wake akiwemo kiungo Marten de Roon.

Mshindi wa mechi kati ya Atalanta na PSG atafuzu nusu fainali ambako huko atakutana na mshindi wa mechi nyingine ya robo fainali kati ya RB Leipzig ya Ujerumani na Atletico Madrid itakayopigwa kesho.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Mpango wa PSG kuelekea ya robo fainali UEFA leo.

Read Next

TAKUKURU yatakiwa kuwadhibiti wanaorubuni wapiga kura.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!