Mgombea Urais nchini Belarus apata hifadhi Lithuania.

Mgombea Urais nchini Belarus katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni, Svetlana Tsikhanouskaya amesema amelazimika kuondoka nchini humo baada ya makabiliano kuibuka kati ya polisi na waandamanaji yaliyosababisha kifo cha muandamanaji mmoja.

Katika ujumbe mfupi aliotuma kwa njia ya video, Tikhano-vskaya mwenye umri wa miaka 37 ambaye anadai kuwa mshindi katika uchaguzi huo, amesema ameamua kutafuta hifadhi nchini Lithuania kutokana na usalama wa watoto wake, jambo ambalo kwake ni muhimu.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Lithuania, Linas Linke-vicius ameliambia shirika la habari la AFP kuwa Svetlana Tikhanovskaya amewasili nchini humo na yuko salama.

Wakati huo huo Poland imesema iko tayari kuwa mpatanishi kati ya Rais Alexander Lukashenko anayetetea nafasi yake katika uchaguzi huo na upinzani. Waziri wa Poland wa mambo ya nje Jacek Czaputowicz amewaambia waandishi habari mjini Riga juu ya utayari huo wa nchi yake baada ya kukutana na mawaziri wenzake kutoka Estonia, Finland na Latvia.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Wafanyabiashara soko la Job Ndugai na Serikali ya mkoa.

Read Next

Serikali (M) Pwani yatenga hekari 40,000 kwa ajili ya wafugaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!