Mpango wa PSG kuelekea ya robo fainali UEFA leo.

Wakati mechi za robo fainali ya michuano ya klabu bingwa Ulaya zikianza leo, Kocha Mkuu wa Klabu ya PSG ya Ufaransa Thomas Tuchel amekiri kuwa timu yake itakabiliwa na mchezo mgumu itakaposhuka dimbani kucheza dhidi ya Atalanta kutokana na kile alichokiita ni uwezo mkubwa wa timu hiyo ya kutoka Italia.

Amesema amejipanga kuhakikisha timu yake inaingia kwa nidhamu ya kimchezo ili kupata matokeo mazuri kwenye mechi hiyo inayopigwa kwenye uwanja wa Luz mjini Libson, na hivyo amelazimika kutengeneza mfumo wa kiushindani ikiwemo wachezaji kujiamini.

PSG imewasili jana mjini Lisbon kwa ajili ya mchezo huo na imefanya mazoezi ikiwa ni maandalizi ya mwisho kuelekea mechi hiyo itakayopigwa leo usiku saa nne kamili, ikiwa na wachezaji wake mahiri akiwemo Neymar, Ander Herera, na Marquinhos.

Kocha Tuchel pia amefafanua suala la Kylian Mbappe ambaye alikuwa anasumbuliwa na majeraha, kwamba iwapo hakutakuwa na athari yeyote ya afya yake baada ya kushiriki sesheni za mazoezi, atajumuishwa kwenye kikosi kitakachoshuka dimbani usiku wa leo.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Serikali (M) Pwani yatenga hekari 40,000 kwa ajili ya wafugaji.

Read Next

Kocha asema timu ya Atalanta itapigana kulinda heshima UEFA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!