Serikali (M) Pwani yatenga hekari 40,000 kwa ajili ya wafugaji.

Serikali mkoa wa Pwani imetenga eneo lenye ukubwa wa hekari elfu 40 kwa ajili ya kulisha mifugo hususan kwa baadhi ya wafugaji ambao wapo katika Bonde la Mto Ruvu katika kukabiliana na migogoro baina ya wakulima na wafugaji mkoani humo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wakati wa ufunguzi wa kikaokazi cha siku moja ambacho kimewashirikisha wakuu wote wa wilaya saba pamoja na wakurugenzi wa halmashauri, wakuu wa idara kwa pamoja ajili ya kujadili changamoto zinazowakabili wananchi

Aidha Ndikilo katika hatua nyingine amewataka wakuu wote wa Wilaya kutoka Mkoa wa Pwani wakurugenzi pamoja na watendaji kuhakikisha wanashughuliakia kero na changamoto mbalimbali ambazo zinakabili wananchi na kuzitafutia ufumbuzi .

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu amesema wamekuwa wakisikiliza kero mbalimbali za wananchi sambamaba na kusuluhisha migogoro ya wakulima na wafugaji pamoja na kushughulikia changamoto ya masuala ya mipaka ya ardhi.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Mgombea Urais nchini Belarus apata hifadhi Lithuania.

Read Next

Mpango wa PSG kuelekea ya robo fainali UEFA leo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!