Shirika la Afya Duniani WHO limesema dawa ya kinga ambayo serikali ya urusi inadai kuigundua, haitaruhusiwa kutumika hadi pale itakapofanyiwa vipimo vya kuthibitisha ubora wake katika maabara za shirika hilo huku urusi ikisema kuwa imeipasisha kwa matumizi kinga hiyo nchini mwake.
Katika tangazo lake hilo,rais Putin amesema nchi yake imekuwa ya kwanza duniani kupata kinga dhidi ya ugonjwa wa covid-19 ambayo amedai ni bora kuliko kinga zozote zilizowahi kutengenezwa duniani na wataipeleka katika maabara ya shirika la afya duniani ili iweze kuanza kutumika maeneo mengine ya dunia.
Kinga hiyo iliyotengenezwa katika maabara ya Gamaleya nchini humo kwa ushirkiano na wizara ya ulinzi ya nchi hiyo ambayo imepewa jina la Sputnik.
Tayari Dawa Kinga 165 zilizotengenezwa katika maabara mbalimbali duniani zipo kwenye majaribio ambapo kati ya hizo 139 zinajaribiwa katika miili ya binadamu.