Tanzania yafanikiwa kutekeleza malengo ya SADC.

Tanzania imesema licha ya kupitia changamoto mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa corona na majanga ya mafuriko imefanikiwa kutimiza malengo waliyokubaliana na nchi wanachama wa jumuiya ya maendeleo kusini mwa afrika SADC huku ikiisihi Msumbiji kuendeleza mafanikio yaliyopatikana pamoja na kutekeleza mkakati na dira ya maendeleo ya Jumuiya hiyo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam na Mawaziri wa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo kupitia mtandao katika kikao cha mawaziri wa SADC kinachoendelea nchini Msumbiji, Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi amesema katika uongozi wa mwaka mmoja, Tanzania imefanikisha kwa kiasi kikubwa malengo yaliyopitishwa na jumuiya hiyo ikiwemo kukifanya kiswahili kuwa lugha rasmi na dhamira ya ujenzi wa viwanda.

Aidha katika kikao hicho kwa njia ya mtandao, Tanzania imekabidhi nafasi ya uenyekiti wa baraza la mawaziri kwa waziri wa mambo ya nje wa Msumbiji.

Kwa upande wake Balozi wa Msumbiji nchini Mhe. Monica Clemente amesema Msumbiji itaendeleza pale ilipoishia Tanzania huku ikitarajia kuitumia Tanzania kama mwalimu katika kutekeleza mipango ya SADC katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wao.

Katika hatua nyingine Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli anatarajiwa kukabidhi nafasi ya uenyekiti wa nchi za Jumuiya za maendeleo ya Kusini mwa Afrika kwa nchi ya Msumbiji Jumatatu ijayo kupitia mkutano wa 40 unaoendelea mjini Maputo Msumbiji.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Maelekezo ya Waziri Jafo hayajafanyiwa kazi.

Read Next

Serikali ya CCM yapanga kununua meli tano kubwa za uvuvi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!