Serikali ya CCM yapanga kununua meli tano kubwa za uvuvi.

Mgombea Mwenza kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema serikali imepanga kununua meli tano kubwa za uvuvi zitakazotumika kuvua samaki katika ukanda wa Pwani.

Mama Samia ambaye pia ni Makamu wa Rais, amesema ununuzi wa meli hizo unalenga kutoa fursa zaidi ya ajira hususani vijana na kuwawezesha Watanzania wanufaike na rasilimali za taifa.

Amesema ununuzi wa meli hizo utakwenda pamoja na ujenzi wa bandari ya uvuvi ambazo meli zote zitakazovua kwenye eneo la bahari ya Tanzania zitatakiwa kutia nanga ili mapato stahiki ya serikali yapatikane.

Akizungumza na wananchi wa Nangurukuru, wakati akiwa njiani kuelekea Mtwara, amesema hatua hiyo itasaidia kuondoa wizi uliokuwa ukifanywa na meli za uvuvi zinazovua samaki ukanda wa bahari ya Tanzania.

Kuhusu shida ya kivuko kutoka Mchinga moja hadi Mchinga mbili, Mama Samia amesema atatuma wataalamu wa vivuko kuangalia eneo hilo ili changamoto hiyo iweze kutatuliwa.

Akizungumza katika mkutano huo, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, wakati akimuombea Kura Mgombea Urais aDkt.John Magufuli amesema wananchi wa Lindi wasubiri neema kutokana na ujio wa ujenzi wa kiwanda cha kuchakata gesi Likong’o ambapo amesema kiwanda hicho kitakuwa na thamani ya dola bilioni 30 ambapo pia mji wa kisasa utajengwa.

Mgombea Ubunge Jimbo la Mchinga (CCM), Salma Kikwete, amesema miradi mbalimbali ya maendeleo imetekelezwa jimboni hapo.akisema sh. bilioni 2.7 zimetolewa na serikali kugharamia elimu bure katika Halmashauri ya Mtama huku sh. bilioni 1.1 zimetumika katika Jimbo la Mchinga.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Tanzania yafanikiwa kutekeleza malengo ya SADC.

Read Next

Watoto watoa Ujumbe wa amani kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!