Dkt. Magufuli aendelea kuinadi ilani akirejea Dodoma.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Tiketi ya CCM Dkt. John Pombe Magufuli amerejea mjini Dodoma baada ya ziara ya kuinadi ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 kwa mamilioni ya wapiga kura wa mikoa ya Pwani na Kaskazini.

Akiwa njiani Kurejea Dodoma akitokea Babati mkoani Manyara amefanya mikutano katika vituo mbalimbali ikiwemo Kondoa, Chemba, Hanette na Veyula.

Katika mikutano yote hiyo Dkt. Magufuli ameyaeleza mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi Cha miaka mitano iliyopita.

Hata hivyo alieleza matarajio ya utekelezaji wa maelekezo ya ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025, ambapo pia ameahidi kuzitatua kero zinazowakabili watanzania kwa ujenzi wa miundo mbinu na huduma za kijamii.

Pamoja hayo Dkt. Magufuli aliwasikiliza wapiga kura hao, huku akiwataka kwenda kupiga kura na kumchagua yeye pamoja na wagombea wote wa CCM.

Hawa hapa Baadhi ya wapiga kura waliojitokeza kumsikiliza Dkt. John Pombe Magufuli.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Mkataba wa kupiga marufuku silaha za nyuklia.

Read Next

Mauzo na manunuzi ya hisa DSE yapanda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!